Beki wa Yanga, Nickson Kibabage Kurudi kwa Waajiri Wake wa Zamani

Beki wa Yanga, Nickson Kibabage Kurudi kwa Waajiri Wake wa Zamani


Beki wa Yanga, Nickson Kibabage ambaye amemaliza mkataba na timu hiyo aliyoitumikia kwa miaka miwili anatajwa kurejea kwa waajiri wake wa zamani Singida Black Stars iliyomnyakua beki wa kulia wa Simba, Kelvin Kijili.

Kibabage alijiunga na Yanga kwa mkopo wa miezi sita na baadae kumnunua mazima kwa mkataba wa miaka miwili ambayo imetamatika mwisho wa msimu huu.

Chanzo cha kuaminika kutoka Yanga kimefunguka kuwa, Kibabage hatakuwa sehemu ya kikosi cha timu hiyo msimu ujao na wapo kwenye mchakato wa kutafuta beki mzawa ambaye atasaidiana na Chadrack Boka.

“Yanga imeingia sokoni inatafuta beki mzawa ambaye atasaidiana na Boka upande huo, kuhusu Kibabage hatakuwa sehemu ya kikosi chetu msimu ujao amemaliza mkataba na sisi. Boka hayupo timamu licha ya kuwa na ubora hivyo anahitaji msaidizi ambaye watagawana mechi ukiangalia tuna mashindano mengi msimu ujao ligi ya ndani, Kombe la Shirikisho (FA) na Ligi ya Mabingwa Afrika.”

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad