BAADA ya Aishi Manula kurejea ndani ya Azam FC akitokea Simba SC matajiri wa Dar wamepiga hodi tena kuulizia uwezekano wa kumpata kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Ladack Chasambi.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari, Azam FC inamtaka kiungo huyo kwa mkopo wa mwaka mmoja katika msimu ujao kwa ajili ya kukiimarisha kikosi hicho.
Simba hadi hivi sasa hawajajibu ofa hiyo waliyopewa na Azam FC kuhusu Chasambi ambaye huitwa mtoto wa maajabu.
Rekodi zinaonyesha kuwa msimu wa 2024/25 alipiga hat trick ya asisti kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar, Uwanja wa Kaitaba.
Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Kagera Sugar 2-5 Simba SC ilikuwa mzunguko wa kwanza