Mobile

MO Dewji Ambakiza Fadlu Davids Simba.....


MO Dewji Ambakiza Fadlu Davids Simba.....


Utata uliokuwapo kuhusu ya hatma ya kocha mkuu wa Simba, Fadlu Davids umemalizwa baada ya chanzo changu kuniambia amekubali kuongeza mkataba mpya wa kuendelea kuinoa timu hiyo aliyoiwezesha kufika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika na kupanda hadi nafasi ya 5 kwa Ubora Afrika.

.

Inaelezwa kuwa, licha ya kocha huyo kuondoka nchini kabla ya kusaini mkataba mpya, mazungumzo yake na bilionea wa klabu hiyo, Mohammed ‘Mo’ Dewji yaliyofanyika juzi yameleta neema kwa Fadlu kukubali kurudi sambamba na benchi lote alilofanya nalo kazi msimu uliomalizika.

.

Chanzo cha ndani kutoka Simba, kimejulisha kuwa, Fadlu pamoja na benchi lote la ufundi wamekubali kusaini mikataba mipya ya mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongezwa mwaka mwingine, baada ya kikao kizito kilichowahusisha viongozi wa juu wa klabu hiyo chini ya Mo Dewji.

.

“Mo Dewji hakutaka kusubiri hata kidogo. Aliamua kukamilisha haraka suala la mkataba mpya kwa Fadlu baada ya kuona kuna mawakala wa timu nyingine wakianza kuwasiliana naye. Mo aliamini kuwa licha ya Simba kutotwaa taji msimu uliopita, kazi ya Fadlu inaonyesha dira sahihi ya mafanikio ya baadaye,” kilisema chanzo changu kutoka ndani ya Simba.

.

Hii ni mara ya pili kwa Mo Dewji kuingilia moja kwa moja masuala ya kiufundi ndani ya Simba katika kipindi cha hivi karibuni, na mara hii akihimiza utekelezaji wa haraka wa ripoti ya kiufundi iliyowasilishwa na Fadlu kuhusu mabadiliko ya kikosi, falsafa ya timu na aina ya wachezaji awatakao.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad