ALI KAMWE: Yanga Hatutaki Kumtambulisha Kocha Mpya Kwa Sasa, Lakini....

ALI KAMWE: Yanga Hatutaki Kumtambulisha Kocha Mpya Kwa Sasa, Lakini....


Ofisa Habari wa Klabu ya Yanga, Ali Kamwe, amesema kuwa klabu hiyo ina bahati msimu huu baada ya kupokea ripoti tatu za tathmini ya kikosi kutoka kwa makocha waliowahi kuifundisha timu hiyo, kuelekea maandalizi ya msimu wa 2025/26. Makocha waliowasilisha ripoti hizo ni Miguel Gamondi, Sead Ramovic na Miloud Hamdi.


Kamwe amesema baada ya kupokea ripoti hizo, hatua ya kwanza iliyochukuliwa na uongozi wa klabu ilikuwa ni kutafuta kocha mpya kwa haraka, ambaye atalingana na falsafa ya Yanga.


Ameeleza kuwa tayari kocha mpya amepatikana na amekabidhiwa ripoti zote tatu kwa ajili ya kuzifanyia tathmini, akilenga kuboresha kikosi kuelekea msimu ujao.

Hata hivyo, Kamwe amesema klabu haitamtambulisha kocha huyo kwa sasa, ili kuepusha presha isiyo ya lazima katika kipindi hiki cha dirisha la usajili.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad