CHELSEA na PSG Vitani Fainali za Kombe la Dunia kwa Klabu

CHELSEA na PSG Vitani Fainali za Kombe la Dunia kwa Klabu


CHELSEA na PSG zimeonyesha kiu yao ya kubeba ubingwa wa fainali za Kombe la Dunia kwa Klabu baada ya kutinga fainali kibabe baada ya kushinda mechi za nusu fainali katika michuano inayoendelea huko Marekani. Baada ya kufika hatua hiyo, timu zote mbili zimejikusanyia mabilioni ya pesa kama zawadi kwa viwango vyao katika michuano hii.

Kwa mujibu wa takwimu hadi sasa timu hizo kila moja imekunja dola 88.43 milioni (Sh 231 bilion). Vilevile wapinzani wao Fluminense imeondoka na dola 60.83 milioni na Real Madrid dola 59.43 milioni ( Sh 156.2 bilioni)

Hata hivyo, kwa upande wa Chelsea na PSG pesa walizopata zinaweza kuongeza kufikia dola 130 milioni ikitegemea na matokeo ya fainali, lakini zote haziwezi kufikia dola 155 milioni hata ikichukua taji hilo kwa sababu tayari ilipoteza mechi moja kati hatua ya makundi, lakini inaweza kufikia dola 130 milioni (Sh 342 Bilioni)

Kiasi hicho cha dola 155 milioni ni mjumuisho ikiwa timu itashinda mechi zote za hatua ya makundi ambapo kila ushindi una zawadi ya dola 2 milioni (Sh 5.2Bilioni) pia ikashinda hatua zinazofuatia hadi fainali.

Mchezo huu wa fainali unatarajiwa kupigwa Jumapili kwenye Uwanja wa MetLife, huko East Rutherford kuanzia saa 4:00 usiku kwa saa za Afrika ya Mashariki.

Tiketi za mechi hii zinaanzia dola 265 kwa baadhi ya tovuti zinazouza lakini kuna tiketi za bei ghali zaidi ambazo zinafikia dola 1500 (Sh 3.9 Milion). Kumekuwa pia na ulanguzi wa tiketi kwa watu wanaonunua kisha kuziuza kwa mashabiki wengine ambapo ripoti zinaeleza kuna watu wanauza tiketi hizo kwa zaidi ya dola 2000.

Rais wa Marekani, Donald Trump anatarajiwa kuhudhuria fainali hiyo ya Jumapili itakayohitimisha michuano hiyo. kwa mwaka 2025.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad