Shaffih Dauda Atia Neno Haji Manara Kudai Pacome Anaenda Kuwa MVP wa Ligi Kuu

 

Shaffih Dauda Atia Neno Haji Manara Kudai Pacome Anaenda Kuwa MVP wa Ligi Kuu


Nimeona video ya aliyekua msemaji wa Yanga, Haji Manara akisema kuwa ‘MVP’ wa msimu huu wa Ligi kuu NBC PREMIER LEAGUE, anaefaa kubeba tuzo hiyo ni Zouzoa Pacome.


Lakini, zipo story mtaani kuwa Jean Charles Ahoua nae ni mmoja wa wachezaji wanaofaa kubeba tuzo hiyo


Takwimu zao msimu huu mpaka sasa— Pacome na Ahoua.


Ahoua: Bao 16, assists 09

Pacome: Bao 11, assists 08


Hizi ndio numbers zao. Kwa kuwa Manara ametufungulia mjadala mzuri, nimeona sio mbaya nikiweka wazi baadhi ya vigezo ambavyo vinatumika duniani kuchagua ‘MVP’ wa ligi husika.


MVP — Kwa maana ya Most Valuable Player huwa kuna vigezo kadhaa (Japo huwa vinabadilika kutokana na Ligi husika)


Individual Perfomance: MVP anaweza kuchaguliwa kwa kuangalia yeye binafsi amefanya nini kwenye ligi husika ndani ya msimu huo. Hapa tunaongelea takwimu kama pasi za mabao, magoli, n.k — Hii ni kwa wale viungo na washambuliaji. Mabeki au kipa tutawapima kwa vigezo vinavyowahusu.


Efficiency & Impact: MVP huweza kuchaguliwa kwa kuzingatia je magoli & pasi zake zina ufanisi na matokeo chanya kwenye timu ambayo anaichezea, Je ameisaidia vp timu yake kushinda vikombe?


Value to the team: Hapa tunampa mchezaji tuzo ya MVP kwa kujiuliza je thamani yake kwenye timu ni ipi kama angekua hayupo?


Consistency & Durability: MVP pia tunampima kwa kuangalia je amekua na muendelezo mzuri wa matokeo chanya kwa msimu mzima.?


Trophies & Awards: Hapa tunaangalia huyu ambae tunataka kumpa tuzo ya MVP ameifanyia nini timu yake? Ameipa makombe mangapi?


Baada ya kuona hvyo vigezo, Je unadhani Manara ana hoja? Je wanaosema Ahoua anafaa wana hoja?


Mimi binafsi naona wachezaji wafuatao wanastahili kugombea tuzo ya MVP: Mousa Camara, Dickson Job, Ahoua, Clement Mzize na Pacome.


Au watu wa boli mnasemaje?

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad