Hapa Ndipo Lilipo Tatizo la Azam Ligi Kuu Licha ya Uwekezaji Mkubwa

Hapa Ndipo Lilipo Tatizo la Azam Ligi Kuu Licha ya Uwekezaji Mkubwa


Tangu mara ya mwisho Kipre Tchetche kuchukua kiatu cha ufungaji bora 2012/13 Azam Fc haijawahi kutoa mfungaji bora tena kwa zaidi ya miaka 10 mpaka sasa.


Ni feisal pekee aliyefukuzana na Stephen Aziz Ki aliyemaliza na magoli 21 msimu pita, Simba na Yanga zimekuwa zikibadilishana tu kutwaa tuzo hiyo miaka na miaka kabla ya George Mpole kufunga magoli 17 mbele ya mkongomani Fiston Mayele (17), Na Ruvu Shooting waliowahi kumuingiza Adbulrahaman Mussa aliye tie na Msuva msimu wa 20216/17


Ili ushinde mechi unatakiwa kufunga magoli kwenye kila mchezo, lakini ili ushinde ubingwa unatakiwa kuwa na safu nzuri ya ulinzi ili ukifunga ulinde ushindi.


Azam kwa miaka 10 haina ngome nzuri ya ulinzi wala safu nzuri ya ushambuliaji licha ya mara kadhaa kuwa na majina makubwa kwenye dirisha la usajili.


Ndiyo maana ukiangalia Azam Fc michezo mingi ametoa sare ama kupoteza ugenini sehemu ambazo mara nyingi timu hazichezi vizuri kwenye open play sababu ya viwanja unalazimika kutumia mipira mirefu kona mipira iliyokufa hapa kama huna washambuliaji wazuri huwezi kupata goli.


Niliandika kuhusu ubovu wa Azam Fc haswa sehemu la ulinzi eneo la mlinda lango wamepitia walinda milango zaidi ya 10 tangu kuondoka kwa Aishi na bado hawajapata mbadala wake hili pia ni eneo linalo waangusha.


Ugenini ndiyo sehemu ambayo Azam Fc ameangusha alama nyingi zaidi kwenye misimu hii mitatu mfululizo kitu ambacho Simba na Yanga wanazichukua na ndiyo sehemu wanapo chukulia ubingwa huko.


Wako mtiifu ✍️ @Cheyolutenganotz

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad