Kama mambo yatakwenda vile ambavyo inazungumzwa kwa sasa, ni wazi kuna nyota kiungo mshambuliaji wa Singida Black Stars, Josaphat Arthur Bauu (22) atatua Jangwan msimu ujao.
Mbali na Bada, pia mshambuliaji wa Singida Black Stars, Jonathan Sowah naye yupo kwenye rada za mabingwa hao watetezi. Chanzo changu cha kuaminika ndani ya Yanga kimeeleza “Ni kweli mazungumzo ya kunasa saini ya kiungo huyo yameanza na yapo katika hatua nzuri, nafikiri kama mambo yataenda sawa atakuwa sehemu ya kikosi chetu msimu ujao kama mchezaji wa ndani baada ya kubadili uraia,” alisema mtoa taarifa huyo na kuongeza
“Tumezingatia mambo mengi kutamani kuwa na mchezaji huyo, ni moja ya wachezaji walioonyesha uwezo mkubwa kwenye ligi yetu, pia tunaamini anaweza kuongeza nguvu kwenye kikosi chetu kutokana na aina yake ya uchezaji,” alisema mtoa taarifa huyo
Bada anamudu kucheza namba nane na 10, kutua kwake ndani ya kikosi hicho itakuwa sehemu ya kuwa mbadala wa Stephane Aziz Ki ambaye anatajwa kuondoka mwishoni mwa msimu.