Chelsea wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Aston Villa Morgan Rogers, mwenye umri wa miaka 22, majira ya kiangazi, wakimtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa England kuimarisha safu yao ya ushambuliaji. (Independent)
Real Madrid wamemweka beki wa Arsenal raia wa Ufaransa William Saliba, 24, kama chaguo lao kuu nafasi ya beki msimu huu wa uhamisho wa kiangazi. (Marca)
Liverpool wanawataka mabeki wa Bournemouth Dean Huijsen, 20, na Milos Kerkez, 21, pamoja na mshambuliaji wa Eintracht Frankfurt Hugo Ekitike, 22, ili kuimarisha kikosi chao na kutetea taji lao la Ligi Kuu. (Daily Mail)
Kiungo wa kati wa Italia Sandro Tonali anapanga kusalia Newcastle United kwa muda mrefu, licha ya kiungo huyo wa miaka 24 kuhusishwa na kurejea nyumbani kwao Italia. (Telegraph)
Manchester City hawana mpango wa kumtoa kwa mkopo kiungo wao wa England Jack Grealish, 29, msimu huu wa kiangazi. (Talksport)
City na Liverpool wana nia ya kumsajili beki wa kulia wa Italia Andrea Cambiaso, 25, ambaye anaonekana kuondoka Juventus msimu huu wa kiangazi. (Calciomercato)
Marcus Rashford huenda akarudi mapema Manchester United kutoka kwa mkopo wake Aston Villa baada ya mshambuliaji huyo wa England mwenye umri wa miaka 27 kupata jeraha la msuli wa paja linaloweza kumuweka nje mpaka mwisho wa msimu. (The Sun)
Rashford yuko tayari kupunguza mshahara wake ili kuondoka United na kufanikisha ndoto yake ya kujiunga na Barcelona. (Mirror)
Lakini kuna changamoto kwani Barca hawako tayari kulipa ada ya £40m iliyokubaliwa na Villa kwa Rashford. (Independent)
Manchester United na Tottenham zote zinamnyatia kiungo mshambuliaji wa Ufaransa Rayan Cherki, 21, kutoka Lyon. (Caught Offside)
Villa wanaripotiwa kuwa tayari kulipa ada ya £21m ya kuvunja mkataba wa kipa wa Hispania Joan Garcia, 23, kutoka Espanyol. (Cadena SER)
Fulham wanahusishwa na beki wa kulia wa Kiingereza Ben Johnson, 25, huku Ipswich ikishuka daraja kutoka Ligi Kuu. (Sky Sports)
Brazil wako katika mazungumzo na meneja wa Real Madrid Carlo Ancelotti kuhusu kuwa kocha wao mpya, huku mazungumzo yakiendelea kuhusu benchi lake la ufundi. (Fabrizio Romano)