Tanzania imeanza vibaya michuano ya UFCON U-20 inayoendelea nchini Misri baada ya kikosi cha timu hiyo kinachonolewa na Charles Mkwasa kupokea kichapo cha 1-0 dhidi ya Afrika Kusini kwenye mchezo wa kundi A uliochezwa kwenye Uwanja wa Suez Canal Jumatano.
Licha ya kutengeneza nafasi nyingi za mabao Tanzania ilishindwa kuliona lango bao pekee la Wasauzi likitiwa kimiani na Shakeel April kipindi cha kwanza ambalo kuihakikishia pointi zote tatu.
Timu ya pili ya CECAFA katika kinyang’anyiro hicho Kenya itamenyana na Morocco katika mechi yao ya ufunguzi ya Kundi B leo.
Washindi wanne wa nusu fainali watafuzu kama wawakilishi wa CAF kwa kombe la Dunia la FIFA la U-20 2025 litakalofanyika Chile.