Mobile

Tetesi za soka Ijumaa: Arsenal wapo kwenye mazungumzo ya kumsajili Zubimendi

 

Tetesi za soka Ijumaa: Arsenal wapo kwenye mazungumzo ya kumsajili Zubimendi

Arsenal imepiga hatua katika mazungumzo ya kumsajili kiungo wa kati wa Real Sociedad na Uhispania Martin Zubimendi, 26, ambaye ana kipengele cha kutolewa cha euro milioni 60 sawa na (pauni milioni 51.2) katika kandarasi yake. (ESPN)

Manchester United inaweza kumtoa mshambuliaji wa Denmark Rasmus Hojlund, 22, kwa Atalanta badala ya mshambuliaji wa Nigeria Ademola Lookman, 27(Sun)

Roma, Napoli na vilabu viwili vya ligi ya Premea vina nia ya kumsajili winga wa Nottingham Forest wa Uingereza Callum Hudson-Odoi, 24, ambaye mkataba wake unamalizika msimu ujao. (Sky Sports)

Newcastle ina nia ya kutumia kipengele cha kuachiliwa kwa pauni milioni 30 katika mkataba wa mshambuliaji wa Ipswich na England wa Chini ya miaka 21 Liam Delap, 22, ambacho kitaanza kuzingatiwa ikiwa Tractor Boys watashushwa daraja kutoka Ligi ya Premia. (Telegraph)

Mshambuliaji wa Wolves Matheus Cunha, 25, yuko tayari kujiunga na Manchester United, ambao wamedhamiria kukamilisha dili la Mbrazili huyo msimu huu wa joto. (Sky Germany).

Tottenham Hotspur itaanza mazungumzo kuhusu kandarasi mpya ya beki wa Argentina Cristian Romero, 26, ambaye anafuatiliwa na Real Madrid na Atletico Madrid. (CaughtOffside)

Atletico Madrid pia wana nia ya kumsajili kiungo wa Tottenham mwenye umri wa miaka 27 na Uruguay Rodrigo Bentancur. (Times)

Kiungo wa Ubelgiji Albert Sambi Lokonga, 25, amepata majeraha manne akichezea Sevilla kwa mkopo msimu huu na anatazamiwa kurejea Arsenal msimu wa kiangazi, huku klabu hiyo ya La Liga ikipania kutumia kumsajili kwa £10.25m. (Mirror)

Kiungo wa kati wa Manchester City na Ubelgiji Kevin de Bruyne, 33, hatacheza Kombe la Dunia la Vilabu la Fifa mwezi Juni kwa kuhofia kuumia na kuhatarisha utafutaji wake wa klabu mpya. (Daily Star)

Tottenham Hotspur wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Manchester United na Uingereza Marcus Rashford, 27, kwa mkataba wa kudumu msimu huu wa joto. (Football transfer)

Wawakilishi wa mshambuliaji wa Real Madrid na Brazil Vinicius Jr wanakanusha kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 anakaribia kusaini mkataba mpya na klabu hiyo. (Athletic)

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad