Simba Wadai Wanaenda Kuanza Upya Afrika Kusini......

Simba Wadai Wanaenda Kuanza Upya Afrika Kusini......


Wakati Rais wa Heshima na Muwekezaji wa Simba SC, Mohamed Dewji Mo, akimkingia kifua kiungo mshambultaj wa timu hivo, Jean Ahoua, nahodha msaidizi wa Wekundu wa Msimbazi, Shomari Kapombe, amesema mpango wao ni kwenda kuanza kazi upya ya kuwakabili Stellenbosch FC wakiwa wamesahau bao moja walilopata nyumbani.

Stellenbosch itaikaribisha Simba SC katika mechi ya marudiano ya hatua ya Nusu Fainali ya Mashindano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho Afrika itakayochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Moses Mabhida, Durban nchini Afrika Kusini.

Simba SC ilipata shindi wa bao 1-0 katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliochezwa Jumapili ilivopita hivyo inahitaji sare ya aina yoyote ili kutinga hatua ya fainali ya michuano hiyo inayoandaliwa na kusimamiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).

Akizungumza na gazeti hili jana, Kapombe, alisema wataingia uwanjani kwenye mechi ya marudiano kama vile hawana chochote mkononi ili iwasaidie kuongeza juhudi ya kupambana zaidi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad