Chalamila Aionya Chadema Kuelekea Kesi ya Tundu Lissu Kesho

Chalamila Aionya Chadema Kuelekea Kesi ya Tundu Lissu Kesho


 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ikitarajiwa kusikiliza Kesi ya Mwenyekiti wa Chadema Taifa Mhe. Tundu Lissu Kesho Alhamisi Aprili 24,2025, Mkuu wa Mkoa wa Dar Es salaam ameonya kuwa anayepanga kuleta vurugu Mkoani hapa ni muhimu akazifanye vurugu hizo nyumbani kwake ama kwenue mkoa anaotokea.


Kauli ya Chalamila imekuja wakati huu ambapo kwenye mitandao ya Kijamii kumeonekana makumi ya watu wakiratibu safari zao kutoka kwenye Mikoa mbalimbali kuja Dar Es salaam kuitikia wito wa Uongozi wa Chadema, waliowataka wanachama na wafuasi wao kukusanyika Kisutu hapo Kesho ili kusikiliza mashtaka ya Lissu.


"Yeyote ama Kiongozi yeyote ambaye hatatii sheria na matakwa yaliyowekwa ashughulikiwe kwa mujibu wa taratibu na kama pia kuna yeyote anayeona kuwa kuna umuhimu wa kuja kufanya vurugu Dar Es salaam tunampatia muda akafanye vurugu nyumbani kwake ama kwenye mkoa anaotokea na kamwe asiharibu amani ya Mkoa wa Dar Es salaam. Huu si wakati wa kuitana kuzungumzia ajenda ya kuleta vurugu." Amesema Chalamila.


Akiziita baadhi ya tabia za wanasiasa kama vyanzo vya kutafuta sifa na huruma za wananchi mara baada ya kufanya mambo yasiyofaa, Chalamila ameonya wananchi kujiepusha kuwa mashabiki wa tabia hizo zisizo njema, akisema zimekuwa na dhamira ya kuua amani ya Tanzania, akiwataka wale wote wasioielewa falsafa ya 4R ya Rais Samia Suluhu Hassan kufuata taratibu nyingine za kisheria zilizopo nchini.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad