Kocha Mkuu wa klabu ya Simba SC amesema kuwa wachezaji wote wa klabu ya Simba SC walionyesha kiwango kibovu katika mchezo wao wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Stellenbosch. Kulingana na taarifa mechi hiyo ilikamilika kwa Simba SC kupata ushindi wa bao 1-0. Mechi hiyo ilichezwa katika uwanja wa New Aman Zanzibar.
Fadlu Davids alisema wachezaji wake kutokana na kiwango kibovu ambacho wachezaji wake walionyesha kwenye mchezo dhidi ya Stellenbosch, mipango yake ilikuwa kumaliza mechi hapa Tanzania lakini wachezaji hawakufanya hivyo na muda huo akawaambia hakuna kuenda mapumziko.
Kwa hiyo wachezaji wake wote walikuwa kwenye kambi ya mazoezi ili kuboresha ubora wao. Ilikuwa ni pigo kubwa kwao kwa sababu hakuna ambaye aliweza kuondoka nyumbani hadi mchezo wa mwisho.
Ikumbukwe kuwa Simba SC leo watasafiri hadi Africa Kusini ili kupambana na Stellenbosch kwenye raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho Afrika. Simba SC ilithibitisha kuwa kikosi cha wachezaji 23 kitaondoka leo.