Yanga wameanza mapema kukifanyia maboresho kikosi chao kuelekea msimu ujao, baada ya kupiga hodi kuulizia huduma ya kiungo mkabaji, James Akaminko kama mbadala mpya wa nyota wao, Khalid Aucho ambaye umri umemtupa sana.
“Nimesikia taarifa hizo, lakini siwezi kueleza chochote bali uongozi wangu (Azam) ndio unajua kila kitu. Kazi yangu ni kucheza soka na naendelea kupambana ili kuhakikisha timu inafikia malengo hayo mengine sio kazi yangu kuyazungumzia,” alisema Akaminko.
Alipoulizwa kama anaweza kujiunga na Yanga, alisema hawezi kuzungumzia, ila anahisi kwamba itakuwa ngumu kwake kwa vile maslahi anayopata Azam ni mazuri zaidi kuliko ofa ya Yanag na pia kiu yake ni kuitumikia kwa muda mrefu na kuipa mafanikio Azam kwa kitendo cha kuaminiwa na kumpa maslahi bor