Tabora United Gari Limewaka...Kila Anaepita Mbele yake Anapigwa Kama yanga



Tabora United imezaliwa upya na hii ni kazi kubwa iliyofanywa na kocha mkuu @kiazmak raia wa Congo.Kocha huyu ni mtaalamu haswa.Katika vitu Tabora watakiwa wajivunie kwa sasa ni kuwa na @kiazmak .Ana mbinu na mikakati bora.Katengeneza utimamu wa mwili wa kikosi chake na kutengeneza mshikamano ndani ya Timu.

Leo KMC FC kapoteza sebuleni kwake tena kwa chumba 2 kwa 0 na kuwafanya Tabora United kubakisha alama 3 kuingia ndani ya Top 4,Kazi kubwa inafanyika na benchi la ufundi chini ya @kiazmak na tangu atue Tabora United hajapoteza mchezo wowote.

Nani alitegemea mwanzoni kama Tabora United kabla hata mzunguko wa kwanza haujamalizika wangekua wanapambania nafasi ya 4 ??? Kazi nzuri @kiazmak 👏👏.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad