No title

 

Rais wa CAF Patrice Motsepe Kuongeza Muhula wa Pili Kama Rais Bila Kupingwa

Patrice Motsepe wa Afrika Kusini anatarajia kurejea kwa muhula wa pili kama Rais wa Shirikisho la soka la Afrika (CAF) baada ya kuwa Mgombea pekee katika nafasi hiyo.


Motsepe alichukua mikoba ya Ahmad Ahmad wa Madagascar Machi 2021 na sasa anatazamiwa kuendelea kuongoza bodi inayosimamia soka barani Afrika baada ya kutokuwa na mpinzani.


Kando na kura ya Urais wa CAF, uchaguzi pia utaamua Wajumbe wapya wa Kamati ya Utendaji ya CAF na Wawakilishi wa Afrika kwenye Baraza la FIFA.


Amaju Pinnick wa Nigeria na Fouzi Lekjaa wa Morocco ni wanachama wa Baraza la FIFA na wanatarajia kutetea viti vyao.


Uchaguzi huo utafanyika Machi 12,2025 huko Cairo, Misri wakati wa Mkutano Mkuu wa CAF.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad