Taarifa iliyotolewa leo November 14,2024 na Uongozi wa Yanga imesema “Vilevile, Uongozi wa Young Africans Sports Club, umesema umesitisha mkataba wa Kocha msaidizi wa kikosi cha kwanza, Moussa Ndaw”
“Uongozi wa Young Africans Sports Club unapenda kuwashukuru Makocha hao kwa mchango wao ndani ya Klabu yetu na unawatakia kila la kheri katika majukumu yao mapya”
“Tayari mchakato wa haraka wa kutafuta Makocha wapya wa kikosi chetu cha kwanza umeanza na unatarajiwa kukamilika hivi punde, Daima Mbele Nyuma Mwiko”