Nyota wa Yanga Stephane Aziz Ki ametemwa katika kikosi cha Timu ya taifa ya Burkina Faso kuelekea katika michezo ya Kufuzu AFCON 2025 nchini Morocco huku Nyota wa Simba Valentin Nouma akijumuishwa katika kikosi hicho.
Burkina Faso watakuwa na kibarua nyumbani Novemba 14 dhidi ya Senegali pamoja na Novemba 18 ugenini dhidi ya Malawi kumbuka kwamba Burkina Faso na Senegal kutoka kundi L tayari wameshafuzu AFCON 2025 ya nchini Morocco.