Kocha Miguel Gamondi Afunguka Sababu za Kufungwa na Azam




Makocha wa timu za Yanga na Azam FC walitoa maoni yao baada ya Azam FC kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Yanga katika mechi ya Ligi Kuu.

Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi, alikiri kushindwa lakini akaeleza kuwa kadi nyekundu iliyotolewa kwa mchezaji wake ndiyo iliyowagharimu zaidi.

"Hakuna anayependa kupoteza lakini inabidi tukubali, hii ni sehemu ya soka," Gamondi alisema,

Aliongeza kuwa, licha ya kucheza pungufu katika kipindi cha pili, timu yake ilionyesha mchezo mzuri zaidi ya Azam, jambo linalowapa matumaini kwa michezo ijayo.

Kwa upande wake, kocha wa Azam FC, Rachid Taousi, alionyesha furaha kubwa kwa ushindi huo, akisema timu yake imekuwa ya kwanza kufunga goli dhidi ya Yanga msimu huu. Alitambua mchango wa kila mmoja aliyehusika katika ushindi huo muhimu.

"Nautoa ushindi huu kama zawadi kwa mashabiki na bosi wetu," alisema Taousi.

Katika mchezo huo uliokuwa wa ushindani mkubwa, kiungo wa Azam FC, Adolf Mutasingwa, alitajwa kuwa mchezaji bora wa mechi na alikabidhiwa tuzo yake kutoka Benki ya NBC.

Mashabiki wa Azam walisherehekea ushindi huu ambao umewapa alama muhimu kwenye msimamo wa ligi, huku Yanga wakijipanga kurekebisha makosa kwa ajili ya mechi zijazo. Mechi ilimalizika kwa matokeo ya Yanga 0-1 Azam.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad