Klabu ya Yanga leo imetangaza rasmi kuachana na aliyekuwa kocha wake Mkuu Miguel Gamondi na kumtangaza kocha mpya Sead Ramovic.
Gamondi ambaye ameiongoza timu hiyo kwenye mechi 40 akishinda 34 akipoteza nne na kutoa sare mechi mbili huku ikifunga mabao 85 na ‘clean sheets’ 27.
Yanga SC, katikati ya Ligi imemfukuza kocha na kumtangaza Sead Ramovic kuwa mrithi wa Gamondi.
Ramovic atafanikiwa kupandikiza falsafa yake kwa Yanga haraka ili iendelee kushinda na itoke kwenye haya machungu inayopitia ya kufungwa mechi mbili mfululizo.
Novemba 26 Yanga watashuka Dimbani kukipiga dhidi ya Al Hilal mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, hatua ya makundi zimesalia siku 10 watafanikiwa kujiandaa vyema na kuelekea mchezo huo?
Tunaweza kusema Yanga wameanza tena kucheza ‘Kamari’ maana uhakika wa kushinda tena itategemea kama wachezaji wataigia kwenye falsafa ya kocha wao mpya Sead Ramovic au uwezo binafsi wa mchezaji mmoja mmoja ili kuipatia ushindi timu yake na sio kama timu?
Presha kwa Wachezaji ipoje kwa wakati huu ambao wanajua wamepoteza mechi mbili mfululizo na kocha kafukuzwa wataweza kuhimili presha mpya kutoka kwa kocha Sead?
Je, itachukua muda gani kwa kocha huyu kuwasoma vyema wachezaji wake na kupandikiza mfumo ambao utakuwa rahisi kueleweka ili timu ipate matokeo mazuri kwa haraka?
Imeandikwa na @itspmshot