Azam Wamecheza Game Bora Sana, Wamestahili Alama 3




Rachid Taoussi alifanya “Home work” yake vizuri dhidi ya Yanga , Azam wakati wanaunda mashambulizi kuanzia chini wanakuwa na muundo wa 2-5-3 , dhumuni lao lilikuwa ni lipi ?

1 : Kutengeneza idadi kubwa ya wachezaji kwenye kiungo “Overload” wakati wakiwa na mali , nafikiri alijua ubora wa Yanga kwenye kiungo ndio maana alihitaji kuwa na wachezaji wengi kwenye kiungo hapo ndio Azam hawakuhitaji nguvu kubwa kuivuka pressing ya Yanga .

2 : Muundo wa kuzuia kwa Yanga bila mpira hakuwa mzuri waliacha nafasi kubwa sana baina ya mchezaji mmoja na mwingine …. Azam walipata nafasi kubwa kwenye mpira hasa wale mawings wao (Nado & Sillah) ni vile tu Azam walikosa utulivu kwenye baadhi ya maamuzi yao .

Yanga wakifika kwenye nusu ya Azam walikosa machaguo sahihi ya pass pia hawakuwa na idadi kubwa ya wachezaji kuifungua defense ya Azam : Nafikiri Azam walifanya home works yao vizuri bila mpira .

Kipindi cha pili , Azam waliamua kuifunga game na muundo wa 4-4-2 bila mpira na wakizuia kwenye “Mid block” waliwafanya Yanga kukosa mianya ya kupitisha mipira ….. Azam walizuia vizuri sana .

NOTE :

Azam wamecheza game bora sana 👏 wamestahili Alama 3 ✅

Feisal “What a player 🔥” amecheza game bora sana 👏 Maestro : akiwa na mali ngumu kuichukua .

Mtasingwa & Akaminko ✅ na wale CB wa Azam 🔥 Yule Sadun “Baller 🔥” . Sillah ✅

Yanga wamefungwa mchezo wa kwanza kwenye ligi msimu huu !.. No Cleansheet kwa Diarra .

Mwamuzi kachezesha vizuri ile ni Red Card ✅

FT : Yanga 0-1 Azam

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad