Yanga Wapokea Kichapo cha Kwanza Ligi Kuu, Bacca Majanga

Yanga wapokea kichapo cha kwanza Ligi Kuu, Bacca majanga

Timu ya Azam FC imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya mabingwa watetezi, Yanga SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.


Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, winga Mgambia, Gibril Sillah dakika ya 33 akimalizia pası ya kiungo mzawa, Adolf Mtasingwa Bitegeko.


Yanga walifungwa bao hilo wakiwa pungufu uwanjani baada ya refa Ahmed Arajiga wa Manyara kumtoa nje kwa kadi nyekundu beki Ibrahim Abdallah Hamad ‘Bacca’ dakika ya 21 kufuatia kumchezea rafu mshambuliaji wa Azam FC, Nassor Saadun Hamoud.


Kwa ushindi huo, Azam FC wanafikisha pointi 21 katika mchezo wa 10, ingawa inabaki nafasi ya nne, wakati Yanga inabaki na pointi 24 za mechi tisa sasa ikiendelea kuongoza Ligi Kuu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad