Taifa Stars jana iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Guinea mchezo uliofanyika nchini Ivory Coast, ukiwa ni wa kuwania kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 2025 nchini Morocco.
Sasa ipo hivi, kwenye makundi mbalimbali ya mitandao ya kijamii hivi sasa wadau wanazungumzia kuhusu benchi la ufundi la Taifa Stars linaloongozwa na Hemedi Suleiman Morocco na wasaidizi wake Juma Mgunda na Jamhuri Kihwelo.
Wapo wanaosema ni wakati mwafaka wapewe timu na wengine wanasema ni mapema, tusubiri kidogo.
Wewe una maoni gani?