KIUNGO wa Yanga na Timuya Taifa ya Tanzania Taifa Stars Mudathir Yahya ametema nyongo kwa wale wanaoibeza timu ya taifa pamoja na wachezaji wake.
Mudathir aliyefunga bao la ushindi dhidi ya Guinea na kuipatia Stars pointi 3 muhimu, alisema kwamba wachezaji wadogo wanaumia na maneno ya Watanzania wanaoibeza timu ya taifa.
“Watanzania wenzetu wanatubeza ila tunashukuru mungu, hatumii bali ndio wanatupa motisha wao wanahisi maneno yao yanatuangusha, wachezaji wadogo wanaumia ila sisi tuliocheza muda mrefu hayatuangushi bali wanatupa nguvu, sisi tunawashukuru kwa maneno yao.”- Mudathir Yahaya