Yanga Yaishushia Mvua ya Magoli Vital'O, Chama Kazaliwa Upya Jangwani

 

Yanga Yaishushia Mvua ya Magoli Vital'O, Chama Kazaliwa Upya Jangwani

Timu ya #Yanga imefuzu kucheza Raundi ya Pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kuifunga Vital’O ya Burundi kwa magoli 6-0 katika mchezo wa pili wa Hatua ya Kwanza.


Mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam unaifanya Yanga kufuzu kwa jumla ya magoli 10-0 kwa kuwa mchezo wa kwanza ilishinda magoli 4-0.


Clatous Chama ameandika rekodi kuwa mchezaji wa kwanza CAF Champions League kutoa assists (4) katika mechi ya leo na kufunga bao 1.


Clatous Chama amehusika kwenye magoli (7) katika mechi (3) za mwisho.


◉ vs Azam FC - Assist 1

◉ vs Vital'O - Bao 1

◉ vs Vital'O - Bao 1 na Assists 4


Full - Yanga 6 - 0 Vital'O


⚽️ Pacome Zouzoua (Pen) — dakika 13'

⚽️ Clement Mzize ›› Assist ya Chama — dakika 48'

⚽️ Clatous Chama — bao dakika ya 50'

⚽️ Prince Dube ›› Assist ya Chama — 71'

⚽️ Aziz Ki ›› Assist ya Chama — dakika ya 79'

⚽ Mudathir Yahya ›› Assist ya Chama dakika ya 84.


Aggregate - 10-0.


Hatua ijayo Yanga itakipiga dhidi ya CBE ya Ethiopia, mchezo wa kwanza Bijana wa Jangwani wakianzia ugenini.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.