Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, Ally Kamwe, amesema kuwa wameandaa ujumbe maalumu kwa ajili ya timu zinazotarajiwa kuwa na nafasi bora ya kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika, wakikabiliana na Vital'0 FC Agosti 24, 2024.
Kamwe ameweka wazi kuwa ujumbe huo utajumuisha mambo mawili makuu: ubora wa kikosi cha Yanga ndani ya uwanja na umuhimu wa kujaza Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa wingi siku ya mchezo wa marudiano hatua ya awali ya mashindano hayo.