Che Malone Gari Limewaka "Nitafunga Sana Msimu Huu"

 

Che Malone Gari Limewaka "Nitafunga Sana Msimu Huu"

Beki wa Simba Che Fondoh Malone ambaye alichaguliwa kuwa mchezaji bora kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tabora United ameweka wazi kuwa mashabiki wanawaogezea ngvu kwenye ushindani kutokana na uwepo wao hivyo waendelee kuwa nao kila wakati.

Mchezo wa kwanza wa ufunguzi kwa Simba ndani ya msimu wa 2024/25 ni Simba ilivuna pointi tatu na kupata mabao matatu kwenye mchezo huo.

Beki huyo alifunga bao la ufunguzi kwa Simba dakika ya 14 kwa pigo la kichwa akiwa ndani ya 18, bao la pili lilifungwa na Valentino Mashaka kamba ya tatu ilifungwa na Awesu Awesu.

Beki huyo amesema: “Ushindi wa Simba ni ushindi wa kila mmoja kutokana na umuhimu wa mashabiki pamoja na kupenda kupata matokeo mazuri kwenye mechi ambazo tunacheza.

“Kikubwa kwa mashabiki waendelee kuwa pamoja kwenye mechi ambazo tunacheza kwani mechi bado zinaendelea na kila timu inaleta ushindani wake ni muda wa kufanya vizuri kwenye mechi zetu zijazo.”

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad