Ali Kamwe Aomba Radhi Kwa Ushindi Mdogo wa Bao 4 Waliopata Yanga Dhidi ya Vitalo......

 

Ali Kamwe Aomba Radhi Kwa Ushindi Mdogo wa Bao 4 Waliopata Yanga Dhidi ya Vitalo......

Kuelekea mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya awali dhidi ya Vital’O ya Burundi, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Young Africans, Ally Kamwe amewaomba mashabiki kuujaza uwanja.


Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Jumamosi ya Agosti 24, 2024 saa 1:00 usiku kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam baada ya ule wa awali kushinda 4-0.


“Matarajio yetu ni kuujaza uwanja wa Benjamini Mkapa kwenye mechi dhidi ya Vital’O. Lakini vilevile tunayo hamasa kubwa ya kufanya vizuri kwenye mchezo huo ni goli la mama.


"Hamasa ya Rais wetu Samia, msimu huu imeanza hatua ya mwanzo kabisa. Sasa hivi tupo kwenye mahesabu ya kuangalia inabidi tufunge magoli mangapi ili tupate hela nyingi. Tunaweza kutafuta mshahara wa wafanyakazi kwenyye goli la mama pekee,” alisema Kamwe na kuongeza.


“Msimu huu tunayo kazi kubwa sana ya kufanya. Kazi ya kwanza sisi kufanya vizuri lakini nimegundua pia tuna kazi kubwa ya kuwaombea wenzetu dua nao wafanye vizuri. Tuna wasiwasi mkubwa sana na mwenendo wa wenzetu kwani matokeo yao hayaridhishi.


“Tuwaombe radhi mashabiki wetu kwa ushindi mdogo tuliopata mchezo uliopita. Kimsingi tunapaswa kushinda magoli mengi sana ili tukombe hizi hela za mama. Uzuri wa hela ya mama haina kona kona, juzi pale Chamazi tumeondoka na milion 20 lakini zingine zilirudi niliona. Zilibaki. Sasa kwanini mtu aje na hela uwanjani aondoke nazo?”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.