KOCHA SIMBA AFUNGUKA 'TUNA TIMU MPYA TUNAENDA KUWAPIGA YANGA BAO'

 

KOCHA SIMBA AFUNGUKA 'TUNA TIMU MPYA TUNAENDA KUWAPIGA YANGA BAO'

Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids amewataka mashabiki na wananchama wa timu hiyo kutokuwa na presha na kusahau kuhusu kipigo cha bao 5-1 walichokipokea msimu uliopita kutoka kwa watani zao, Yanga SC.


Fadlu ambaye amejiunga na Simba msimu huu amesema kuwa mchezo wa kesho wa Ngao ya jamii dhidi ya Yanga watauendea kama michezo mingine yoyote na kulingana na mipango yake pamoja na uwezo wa wachezaji wake, anaamini watapata ushindi.


"Simba Day imetuonesha njia wapi tunaekelea na sasa, hasa mechi iliyopita (dhidi ya APR) kipimdi cha pili. Tumemaliza wiki ya nne ya maandalizi (pre-season) na tunakwenda kucheza na Yanga ambao ni mabingwa wa Ligi. Ni mechi ngumu, tunaichukulia kama mechi nyingine yoyote, hakuna utofauti, malengo yetu ni ushindi.


"Nina uzoefu wa dabi nyingi nah ii ni miongoni mwa dabi kubwa barani Afrika. Tutaiendea mechi hii kwa ukubwa. Nafahamu msimu uliopita mashabiki waliumia kwa kupoteza michezo yote ya Ligi dhidi ya Yanga, bao 5-1 na bao 2-1, lakini hii ni timu mpya na mpango wetu ni mpya, tunaamini tutashinda.


"Mechi iliyopita tulionesha uwezo mkubwa kipindi cha pili, wachezaji wageni ni kama timu iliyokuwepo muda mrefu, sisemi kama ndivyo itakavyokuwa kwenye mchezo dhidi ya Yanga bali tutaendelea kuboresha siku hadi siku, mechi hadi mechi ili kupata kile tunachokitaka," amesema Fadlu

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.