PACOME AHAIDI MAKUBWA MCHEZO WA LEO SIMBA NA YANGA 'NITAWALA CHENGA SANA'

 

PACOME AHAIDI MAKUBWA MCHEZO WA LEO SIMBA NA YANGA 'NITAWALA CHENGA SANA'

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Pacome Zouzoua (katikati) akiwatoka wachezaji wa Red Arrows wakati wa mechi ya kirafiki iliyochezwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Agosti 4, 2024. Picha na Loveness Bernard


Kuelekea katika mechi ya dabi itakayochezwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, kiungo wa Yanga Pacome Zouzoua amefunguka kuhusu mwanzo wake mpya.


Kupitia Mwananchi iliwahi kuwatarifu mashabiki kuwa, kocha wa kikosi hicho, Miguel Gamondi ameweka wazi kuwa katika mechi hiyo hataangalia majina makubwa ya wachezaji, lakini ubora wa wachezaji.


Akizungumza na Mwananchi, staa huyo wa kimataifa wa Ivory Coast amesema kuwa anataka mashabiki wa Yanga wafurahie kipaji chake na kwa kuanzia anataka kuonyesha kwenye  mchezo wa Agosti 8 dhidi ya Simba.


Ameeleza kuwa licha ya ushindani wa namba ndani ya timu  kuwa mkubwa, lakini anataka kuwa na kitu tofauti ili kuhakikisha kwamba anapata nafasi ya kufanya makubwa.


"Mchezo dhidi ya Simba utakuwa mgumu kutokana na wapinzani wao, kwani wamesajili wachezaji wazuri wenye ubora na rekodi za maana walikotoka.


"Lakini sisi kama wachezaji tunatambua umuhimu wa matokeo mazuri kwenye mchezo mkubwa kama huo kwa kipindi cha mwaka mmoja nilichokuwa ndani ya Yanga," anasema kiungo huyo.


Ikumbukwe kuwa Pacome ni miongoni mwa wachezaji waliocheza mechi za Dabi msimu uliopita baada ya kuwafunga Simba mabao 7-2 katika mechi mbili.


Licha ya rekodi hiyo, Yanga inaingia katika mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya kufungwa na Simba ambayo ndiyo bingwa mtetezi wa Ngao ya Jamii.


Hata hivyo, msimu uliopita haukuwa mzuri kwa nyota huyo licha ya kufunga mabao saba na asisti nne, kwani majeraha yalimfanya kushindwa kucheza mechi mbili muhimu za robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.