Eng. Hersi: Siogopi Yanga kufungiwa na FIFA

 

Eng. Hersi: Siogopi Yanga kufungiwa na FIFA

Rais wa Klabu ya Yanga, Eng Hersi Said amesema kuwa haogopi timu yake kufungiwa na FIFA kusajili kwani anachokifanya kuchelewesha malipo ya wachezaji wanaovunja mikataba na klabu ni kutokana na vipaumbele ambavyo wao kama viongozi wa timu wanakuwa wamevipanga.


Hersi amesema hayo kutokana na mijadala mingi kuibuka kuwa Yanga imekuwa ikifungiwa mara kwa mara kwa kushindwa kumalizana na wachezaji vizuri hasa wanapofanya maamuzi ya kuwavunjia mikataba yao na kuwaondosha klabuni bila kumaliza kuwalipa stahiki zao.


“Mimi huwa nashangaa sana watu wanaosema Yanga wamefungiwa kusajili kama vile ni kitu cha ajabu,utakuta mtu kaandika kichwa cha habari kikubwa "YANGA KAFUNGIWA KUSAJILI" kafungiwa jela au..!! Mimi siogopi Yanga kufungiwa na wala sio kitu cha ajabu klabu kufungiwa,kuna klabu nyingi sana duniani zinafungiwa kusajili ni jambo la kawaida.


“Siwezi kulipa mchezaji kwa kuogopa kufungiwa wakati tuna mambo mengine mengi sana ya umuhimu tunapaswa kuyafanya, juzi tu hapa rais wa TP Mazembe, Moise Katumbi alinipigia simu kwamba wana kesi na Ramadhani Singano ‘Messi’ ambayo wanahitaji kulipa pesa akawa anaulizia kama anaweza pata pesa ya biashara tuliyofanya na Baleke.


“Licha ya sisi kuonekana tunafungiwa lakini hakuna msimu ambao tumewahi kuanza msimu bila kusajili,unanifungia sasa hivi wakati usajili umefungwa sasa nalipaje pesa wakati bajeti yangu nahitaji kusafirisha timu kwenda kucheza klabu bingwa," amesema Eng. Hersi Said.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.