Kocha wa zamani wa Simba SC Patrick Aussems “Uchebe” (59) Raia was Ubelgiji ametangazwa kuwa Kocha mpya wa Singida Black Stars kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Aussems ambaye ana uzoefu wa soka la Afrika Mashariki aliifundisha Simba SC msimu wa 2018/19 na kisha kutimkia Black Leopards ya Afrika Kusini.