Kocha Afichua Usajili wa Inonga FAR Rabat, Kumbe Alimalizana nao Kitamboo

 

Kocha Afichua Usajili wa Inonga FAR Rabat, Kumbe Alimalizana nao Kitamboo
Kocha Nabi na Inonga

KOCHA wa zamani wa Yanga, Nasreddine Nabi amesema wala sio ishu mpya kwa beki Mkongomani kusajiliwa FAR Rabat ya Morocco, kwani jamaa alishamalizana nao kitambo kisha akasema atapiga kazi ya maana.

Inonga inaelezwa amesaini miaka mitatu ya kuichezea timu hiyo aliyokuwa akiinoa Nabi na kuifanya imalize nafasi ya pili, ikiukosa kiduchu ubingwa mbele ya Raja Casabalanca na tayari Simba ilishampa mkono wa kwaheri baada ya kulikamilisha dili hilo la FAR iliyowauzia, kwani ilikuwa na mkataba naye.

Nabi ambaye anaondoka FAR Rabat anayotua Inonga akijianda kutua Afrika Kusini kujiunga na Kaizer Chiefs, alisema alitamani kufanya kazi na beki huyo lakini haikuwa rahisi.

Nabi alisema wakati anafika Rabat alikuta taarifa za beki huyo kusaini timu hiyo mapema, kisha pande hizo mbili kukubaliana kusogeza mbele muda wa Mkongomani huyo kujiunga.

“Inonga ni beki mzuri sana sio rahisi kwa mchezaji kucheza Tanzania na kupata nafasi katika kikosi cha DR Congo tena akiwaweka nje mabeki wanaocheza soka la Ulaya,” alisema Nabi na kuongeza:

“Nilikuwa natamani kufanya naye kazi (Inonga) lakini nadhani anakuja hapa wakati ambao nimekuwa na maamuzi tofauti lakinio naamini kwamba FAR Rabat imepata beki mzuri.”

Pia Nabi alisema beki huyo atakuwa nguzo muhimu ndani ya Rabat kwani msimu uliopita alikuwa na kiu ya kuwa na mlinzi kama huyo baada ya beki mmoja tegemeo kukumbana na majeraha ya muda mrefu.

“Inonga ni mpambanaji wakati huu anajiunga pale naamini anakwenda kujiunga na timu sahihi, msimu huu unaokwisha nilitamani angekuwa amefika kwa kuwa kuna beki aliumia kumkosa imetugharimu sana kuchangia hata kukosa ubingwa.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.