Bajeti ya Yanga si Mchezo Bilioni 24.5 , Simba Bado Hawajielewi

 

Bajeti ya Yanga si Mchezo Bilioni 24.5 , Simba Bado Hawajielewi

MABINGWA wa Ligi kuu na Kombe la Shirikisho Yanga SC wametaja bajeti ya klabu hyio kwa msmu uliopita, ambapo kwa msimu ujao Bajeti yao wanatarajia kuwa ni Bilioni 24.5.

Katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Yanga, kila kitu kinawekwa wazi na mipago ya msimu ujao ikiendelea kupangwa huku upande wa pili, Simba SC mamb ndiyo kwanza yanakuwa meusi, migogoro kila kukicha hii inatoa taswira mbaya sana kwa klabu hiyo iliyopoteana kwa misimu mitatu sasa.

MCHANGANUO WA MAPATO YA YANGA MSIMU 2023/24

Udhamini na haki za matangazao bilioni 10.19

Mapato mlangoni bilioni 1

Ada za Wanachama milioni 613

Zawadi za ushindi bilioni 3.9

Mapato mengine bilioni 5

Jumla ya mapato ni Bilioni 21

Bajeti ya Msimu ujao ni Bilioni 24.5 ambapo imeongezeka asilimia kumi tofauti na Msimu uliopita ambayo ni Bilioni 22.

Kwa dalili hizi ambazo Yanga wameanza kunesha, huenda wakafanikiwa zaidi ndani ya uwanja kwa msimu ujao, kiusajili  na kutwaa mataji ya ndani na huenda hata Kimataifa wakafanya vizuri zaidi,  japo kwenye mpira sio pesa tuinafanya kazi bali na mipango thabiti, kitu ambacho Yanga wanacho.

Upande wa pili  Simba wao wamendelea kuvutana mashati na hawajui   mchawi wao ni nani, baadhi ya wananchama wanasema ni muwekezaji, huku wengine wakisema ni Viongozi wa klabu hiyo, hii haitoi mwanga wa matumaini kwa Simba ambaye alishapoteana misimu mitatu nyuma.

Kama mambo yataendelea kwenda kama hivi, basi Simba itazidi  kudidimia kama sio kuzama kabisa baharini

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.