Kigwangala : Mo Dewji Aondoke Haidai Chochote Klabu ya Simba kwa Mujibu wa Mkataba




Mwanachama wa klabu ya Simba Hamis Kigwangala [MB] ameweka wazi kuwa Mohamed Dewji haidai chochote klabu ya Simba kwa mujibu wa mkataba.

Kigwangala amemtaka pia mwenyekiti wa klabu hiyo kuitisha kikao cha wanachama ili wajue mapato na matumizi ya klabu hiyo huku akieleza kuwa bodi iliyowekwa na mwekezaji ni genge la wapigaji.

“Ile bodi ilikuwa genge la watu walioiteka tu timu yetu kinyemela. Kwa taarifa za Ndg. Issa, maana yake Glezabhai hana haki wala mamlaka yoyote yale kisheria kwenye Simba. Simba SC ni club ya wanachama kwa asilimia 100.

“Wanachama tunamtaka Ndg. Mangungu aitishe mkutano mkuu haraka tuamue hatma ya club yetu. Kwenye mkutano huo aandae hesabu za mapato na matumizi ya Simba….kuanzia viingilio vya getini siku za mechi, mikataba ya mauzo ya bidhaa, mikataba ya mauzo ya haki za matangazo (ikiwemo ya bidhaa za Glezabhai, mbet nk), mapato ya CAF (robo fainali zote), n.k.

“Ndg. Mangungu na Kamati Tendaji wakishindwa kufanya hivi, tutaingilia kati kwa kuunda ‘kikosi kazi’ maalum (task force) cha kuiokoa club yetu.”

- Hamis Kigwangala [MB], Mwañachama wa klabu ya Simba.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.