Rais wa Young Africans SC, Eng. Hersi Said, amefichua kwamba, ujenzi wa uwanja wa Klabu hiyo uliopo Makao Makuu ya Klabu, Jangwani, utaanza muda wowote kuanzia sasa.
Eng. Hersi amebainisha kwamba, kinachosubiriwa kwa sasa ni majibu ya barua ya mwisho ya uongozi iliyotumwa kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mohamed Mchengerwa, ikijibiwa na kupatika ardhi yetu, kazi inaanza haraka.
“Tumefanya taratibu zote na barua tumeituma ipo kwa mheshimiwa Mchengerwa ambaye anasimamia Wizara ya Tamisemi na kupitia hapo kuna Tarura waliopewa mradi wa pale Jangwani.
“Baada ya hapo tukishapewa ardhi yetu, Ghalib Said Mohamed (GSM) alionesha nia ya kuwa mmoja wa washirika wa ujenzi wa uwanja na maandalizi upande wake yameshakamilika, tunachosubiri ni kuruhusiwa na Serikali kupitia wizara kupewa ardhi hiyo.
“Niwaambie tu kwamba, siku ambayo tukipata majibu ya barua hiyo ya mwisho, siku inayofuata tutaanza ujenzi,” alisema Eng. Hersi.