SIMBA UBINGWA LIGI KUU BYE BYE…KUSHIRIKI KLABU BINGWA AFRIKA YAGEUKA NDOTO


Dakika 90 zimemalizika katika Dimba la Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi kati ya Namungo ‘The Southern Killer’ na Simba SC huku mchezo huo ukimalizika kwa sare ya bao 2-2.

Simba ndiyo walikuwa wa kwanza kufunga bao la kwanza kupitia kwa Willy Esomba Onana kabla ya Kelvin Kongwe Sabato kuisawazishia namungo dakika nne baadaye (dakika ya 39), na kufanya ubao usome bao 1-1 mpaka dakika 45 za kwanza zinamalizika.

Kipindi cha pili Simba waliingia kwa kasi kusaka bao la pili ambapo waliwalazimisha Namungo kufanya makosa ambayo yaliwafaidisha Simba kwa free kick ya Edwin Balua iliyozama langoni moja kwa moja na kumshinda mlinda mlango, Jonathan Nahimana dakika ya 69
.
Namungo walicharuka na kurudi kwa kasi wakisaka bao la kuwasazisha, mpira uliopigwa na mshambuliaji Meddie Kagera na kumfanya beki wa Simba, kennedy Juma kujifunga dakika ya 90.

Kwa matokeo hayo, Simba anabaki pale pale kwenye msimamo akiwa nafasi ya 3 akiwa na alama 47 katika michezo 22 aliyocheza huku Namungo akiwa nafasi ya 9 na alama 27 katika michezo 24 aliyocheza

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.