Kimoyo moyo Benchikha Anajuta Kukubali Kuja Kuifundisha Simba....


Kocha Bechikha
Kocha Bechikha

Bechikha ni kocha wa makombe,kabla ya kuja Simba alipita kwenye timu (24) tofauti na huko alifanya balaa.

Mfano akiwa Club Africain ya Tunisia alifanikiwa kuwapa ubingwa wa ligi kuu na FA,Tukumbukuke Club Africain siyo Du Sahel wala De Tunis,lakini Benchikha aliwaheshimisha.

Akiwa Difaa Hassan El Jadida,alifanikiwa kuwapa ubingwa wa (FA) tena mbele ya Widad na Raja.

Akaenda Berkane akawapa ubingwa wa Super Cup mbele ya Widad,bingwa mtetezi wa CAF Champions league.

Wote tunakumbuka alichofanya msimu uliopita akiwa na USM Alger,maana aliwapa ubingwa wa Shirikisho mbele ya Yanga na ubingwa wa Super Cup mbele ya Al Ahly.

Benchikha ni “serial winner” kama ukimpatia wachezaji wa maana✍️

Yeye anahitaji vitendea kazi ili ukupatie vikombe✍️

Ameshinda vikombe akiwa na timu ndogo na kubwa,Tactically he’s very good🔥

Leo muda mwingi nimemuona akilalamika na kushika kichwa,kwa kifupi wachezaji wanamuangusha,kila siku kwenye uwanja wa mazoezi anawambia nini cha kufanya ila wakiingia uwanjani wanafanya yao.

Inawezekana kimoyo moyo Benchikha anajuta kukubali project ya Simba✍️

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.