Rais klabu ya Yanga, Hersi Said amesema wakati wa usajili kama muhusika asipokuwa na uelewa kuhusu wachezaji anaweza kumsajili hovyo ama kufukuza wachezaji bila sababu ya msingi.
Hersi amesema hayo kupitia moja ya mahojiano na redio moja leo Jumatatu Aprili 29, 2024 akidai kuwa usajili ni sanaa ni lazima ujue kwanini unasajili hivyo hauwezi kukaa na wachezaji wazuri muda wote bali unapaswa kutengeneza mazingira mazuri ya kuwavutia wachezaji wengine.
“Unapokuwa Kiongozi lazima uwe na maono makubwa sana na uelewa mkubwa wa mpira. Unapaswa kujua mchezaji yupo kwenye kilele cha ubora wake, anapata wakati mgumu kuzoea mazingira au amechoka. Usipokuwa na uelewa wa mpira basi utajikuta unasajili hovyo au unatimua wachezaji kwa hisia” amesema Hersi
Pia, amesema unapokuwa kiongozi lazima uwe na maono makubwa ambayo yatasaidia kujua mchezaji yupo katika ubora wake na wakati mgumu kuzoea mazingira pindi anapokuja kucheza katika timu.