Zimbwe: Nimebeba makombe yote ya nchi hii

Zimbwe: Nimebeba makombe yote ya nchi hii

Beki wa pembeni wa Simba SC, Mohamed Hussein amesema anajivunia kubeba makombe yote ya nchi hii kwa nyakati tofauti.

Mohamed ameyasema hayo jana mara baada ya kuibuka washindi katika mchezo wa fainali ya Kombe la Muungano.

"Furaha yangu ni kuchukua kombe la muungano ambalo nilikuwa nalisikia tu kwenye historia ya mpira wetu kipindi nipo mdogo, namimi nimeingia kwenye hiyo historia, kwa ufupi nimechukua makombe yote ya nchii hii, Shukrani Fans wetu endeleeni kutusapoti," aliandika Mohamed Hussein aka Zimbwe Junior.

 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.