Aprili 20 Nawaambi Yanga Atapigwa na Simba Hamta Amini - Justine Kessy

Aprili 20, Yanga atapigwa na Simba - Justine Kessy


Mtangazaji wa Mjini FM, Justine Kessy amesema kuwa Klabu ya Yanga isipokuwa makini kwenye mchezo wao wa dabi huenda wakapoteza dhidi ya Simba SC, Jumamosi, Aprili 20.


Justine amesema kuwa Simba wanayo nafasi kubwa ya kushindwa mchezo huo kwa kuwa ni mechi yao ya kufa na kupona ili kurejesha morali ya kikosi chao baada ya kupoteza mechi nne mfululizo.


“Huwa wanasema dabi haina mwenyewe ila sio kwa dabi hii… mimi naona matokeo ya Yanga ni mawili tu, asipotoa sare basi atapoteza huo mchezo. Ubora wa Yanga unanikataa kabisa, inawezekana ikawa ndiyo mechi pekee ambayo Simba wata-turn point yao.


“Simba wanajua baada ya mchezo huo wakifungwa wao watadhalilika, Yanga akipata ushindi watu hawatatoka kwa Mkapa, atawadhalilisha na watu watakesha uwanjani kama Simba alivyotoa sare na ASES Mimosas.


“Tukija kwenye uhalisia wa soka, Simba anaweza kushika bomba na amewahi kuwashika Yanga tena ya nabi na akapata matokeo. Zile tano alifungwa Robertinho sio Benchikha, anaweza kupaki basi halafu bahati bahati bao akafunga mtu kama Fredy Michael na mechi ikaishia hapo.


“Yanga kwa vile wapo bora sana kwa sasa wanaweza kupata matokeo mazuri sana ikawa udhalilishaji kwa Simba, lakini kama Simba watakwenda kwa adabu kama Yanga waliyoitumia kwenye mechi za Mamelodi zote mbili, basi huenda Yanga akatoa sare au akafungwa ushindi mwembamba.


“Simba ajitahidi tu kushikilia bo,ba hapa na tunduma, lakini akina Chama wakileta jeuri ya kupishana na kina Aziz Ki, watawapiga nyingi,” amesema Justine Kessy.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.