Bao 5 Chache, Simba Wakitoa Sare Aprili 20 Wachinje ngamia saba

Bao 5 chache, Simba wakitoa sare Aprili 20 wachinje ngamia saba« NyumaMbele »Comments (0)Listen to Article


Aliyekuwa Msemaji wa Klabu ya Yanga, Haji Manara amesema kuwa iwapo hakutakuwa na mambo mengine nje ya uwanja badi timu hiyo itawafunga watani zao Simba SC zaidi ya bao 5 kwenye mchezo wa Aprili 20.


Yanga wanatarajia kushuka dimbani dhidi ya Simba huku wakiwa na kumbukumbu ya kuwatungua watani zao bao 5-1 mwezi Novemba mwaka jana.


“Ukiachana na mambo ya bahati, kujiamini na mambo mengine, kwa imani yangu ukienda uwanjani kwenye uhalisia, yani kama mechi inaamriwa tu na ubora wa timu, hamsa (bao tano) chache. Yanga unawaona wanavyocheza?


“Juzi Mwanza wamecheza kwenye tope kama sangara. Ukimuone yule Aziz Ki sasa hivi, shida. Siwatishi, ile mechi ya dabi Pacome ndani, Aucho ndani, Yao ndani. Yule Mzize hatari, kama mechi inachezwa bila kutegemea mambo ya bahati, zikifungwa bao tano basi chache.


“Simba akipata sare hii mechi asichinje mbuzi kwa sababu mbuzi ni mnyama zaifu kwenye kafara, wakipata droo wachinje ngamia saba kwa sababu ni bahati. Hivi umewaona Yanga lakini au nyie mnazungumzia Yanga ipi?,” amesema Manara.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.