Simba ni Klabu Tajiri, Tusiwachukulie Poa - Wakili Yanga

 

Simba ni Klabu Tajiri, Tusiwachukulie Poa - Wakili Yanga

Mkurugenzi wa Sheria wa Yanga, Wakili Simon Patrick amewataka mashabiki wa timu hiyo wasiwachukulie poa watani zao Simba Sc kwani wana kikosi bora licha ya kupata matokeo mabovu kwa mechi za hivi karibuni.


Wakili Patrick amesema hayo kuelekea mchezo wao wa dabi ya Kariakoo dhidi ya Simba utakaopigwa kesho Aprili 20, 2024 katika Dimba la Mkapa majira ya saa 11:00 jioni.


"Ndugu zangu Wananchi, msikubali kudanganywa na kuuona mchezo wa derby wa Jumamosi kama rahisi.


"Naomba tuwe wakweli, watani zetu wana kikosi kizuri kuliko timu yoyote kwenye ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati, na ndio timu tajiri namba 3 Afrika huku wana wachezaji waliozoea kuwakaba wakina Ronaldo.


"Naomba tujitokeze kwa wingi tuisapoti timu yetu kwenye mchezo huu mgumu! Wazee wetu wa Yanga, tumewakabidhi roho zetu, kila la kheri Jumamosi.


"NB: Umuhimu wa mtu huonekana pale ukishampoteza, endeleeni kumchukulia poa Mzee wetu Mangungu," amesema Wakili Simon.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.