Sare na Coastal Union Yaipeleka Timu ya Azam Kileleni, Fei Toto Aendeleza Moto

Sare na Coastal Union Yaipeleka Timu ya Azam Kileleni, Fei Toto Aendeleza Moto


Timu ya soka ya Azam FC imeendelea kudondosha alama baada ya kukubali kutoa sare ya bao 1-1 dhidi ya Coastal Union ya Tanga katika Dimba la Azam Complex Chamazi Dar jioni ya leo Jumatano, Machi 6, 2024.


Matokeo ya mchezo huo wa raundi ya 20 kwa Azam umeifanya Azam kujikita kileleni mwa Ligi Kuu ya NBC ikiwa na alama 44 mbele ya Yanga ambao wapo nafasi ya pili na alama 43 huku wakiwa na michezo 16 pekee waliyocheza mpaka sasa na Simba nafasi ya tatu wakiwa na alama zao 36 na michezo 16.


Coastal ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao la uongozi kupitia kwa Charles Semfuko dakika ya 67 ya mchezo kabla ya kiungo wa Azam, Feisal Salum 'Fei Toto' kusawadhisha dakika ya 80 ya mchezo.


Licha ya Azam kubanwa mbavu, Fei Toto ameendelea kujikita kileleni kwenye orodha ya wafungaji bora baada ya kufikisha mabao 12 mbele ya Aziz Ki wa Yanga mwenye mabao 10.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad