Hasheem Ibwe: Yanga Bingwa, Azam FC nafasi ya pili


M


semaji wa Klabu ya Azam, Hasheem Ibwe amesema kuwa licha ya kutoa sare kwenye mechi za hivi karibuni, kikosi chao kipo vizuri na bado wanayo matumaini makubwa kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC msimu huu.


Ibwe amesema hayo baada ya kumalizika kwa mchezo wao dhidi ya Coastal Union jana na kuambulia sare ya bao 1-1 huku akiwapiga dongo Simba SC kuwa hawana timu na hawataweza kumaliza nafasi mbili za juu kwenye msimamo wa Ligi.


“Prisons noma, wale jamaa ni hatari, wanapiga kwenye ugoko tu, aliyekuwa anamuuliza Simon Mbangula kamuona sasa, sio Samson wa Delila yule ni Samson mwenyewe, kwa kweli nimefurahi sana Simba kufungwa.


“Simba msimu huu wanautoa wapi? Wa kwanza yanga wa pili mimi (Azam FC). Watafute friji kubwa ili watunze viporo visichache, vinginevyo hama timu pale,” amesema Ibwe

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.