Prince Dube Arudisha Kila Kitu Alichopewa na Azam FC

  

Prince Dube Arudisha Kila Kitu Alichopewa na Azam FC
Prince Dube Arudisha Kila Kitu Alichopewa na Azam FC

Wakati Sakata la Mshambuliaji wa Azam FC Prince Dube likiwa bado linapamba moto, Mwandishi wa Michezo kutoka kituo cha Efm Jemedari Said kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika;


"Kuna taarifa kwamba mchezaji wa Azam FC PRINCE DUBE amerejesha kilakitu alichopewa na klabu yake ya Azam ikiwemo nyumba, ikiwa ishara ya kusisitiza kutaka kuondoka kwenye klabu hiyo.


Dube ambaye hakuwepo kwenye mazoezi ya leo alikuwepo jana na hakwenda kimazoezi ila alifanya maongezi na kocha Dabo tu, jambo ambalo wenzie walipata imani kwamba leo angerejea mazoezini.


Wakati huo huo pia taarifa zinasema wachezaji wengi wamechukizwa na kinachoendelea kwakuwa wanajua sakata la Dube limekuwa la muda mrefu kiasi, lakini kufikia kuandika barua wanaona kama limezidi mpaka na hawamuoni kama mwenye moyo na timu hiyo tena.


Kama hili la kurejesha mali za klabu litakuwa kweli basi manake sakata hili litakuwa limepiga hatua kubwa sana kuelekea ndoa kuvunjika kati ya Dube na Azam FC. Kwakuwa ni hatari sana kuwa na mchezaji ambaye moyo wake hauko kwenye timu na ameshafanya maamuzi mengine juu ya maisha yake klabuni kwenu.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.