MATOKEO Yanga Vs Geita Gold Mine , 14 March 2024

MATOKEO Yanga Vs Geita Gold Mine , 14 March 2024


Bao pekee la kiungo Mburkinabe, Stephane Aziz Ki dakika ya 28 limeipa Yanga SC ushindi wa 1-0 dhidi ya Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.


Kwa ushindi huo, mabingwa hao watetezi, Yanga wanafikisha pointi 52 katika mchezo wa 19 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi nane zaidi ya Azam FC wanaofuatia ambao pia wamecheza mechi moja zaidi.


Kwa upande wao, Geita Gold baada ya kupoteza mchezo wa leo wanabaki na pointi zao 21 za mechi 21 sasa nafasi ya 13 kwenye ligi ya timu 16, ambayo mwisho wa msimu mbili zitashuka na mbili zitamenyana zenyewe ili moja ibaki Ligi Kuu.


Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu ya Championship kujaribu tena kurudi Ligi Kuu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.