Kiungo wa Yanga, Khalid Aucho Aucho Avunja Ukimya Ishu ya Kupasuliwa Goti
Kiungo wa Yanga, Khalid Aucho amevunja ukimya ikiwa ni saa chache tangu afanyiwe upasuaji na kuwashukuru mashabiki, wachezaji na viongozi wa timu hiyo wanaomfariji kipindi hiki anachopitia changamoto ya kuuguza goti huku akiwatoa hofu kuwa atarudi hivi karibuni akiwa bora.
Aucho ameyasema hayo siku moja baada ya kufanyiwa upasuaji mdogo wa goti huku akitakiwa kukaa nje kwa muda wa wiki tatu na kumfanya akose mechi tatu za Ligi Kuu Bara na kuwa kwenye hatihati ya kucheza mechi ya kwanza ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo droo yake inatarajiwa kupangwa Jumatano ijayo ya Machi 12.
Katika mtandao wa kijamii wa Yanga, Instagram' Aucho amewashukuru mashabiki wa timu hiyo huku akiwatoa hofu kwa kuwaambia anaamini atarudi akiwa bora zaidi kuipambania timu.
"Asanteni kwa jumbe zenu za pole, nawashukuru sana, naendelea vizuri sasa natarajia kurudi nikiwa bora zaidi tayari kwa ajili ya kuipambania timu," amesema Aucho aliye na msimu mzuri akiwa na kiwango cha juu kilichomfanya awe tegemeo kwenye eneo hilo la kiungo cha ukabaji.
Baadhi ya viongozi waliomtembelea kiungo huyo ni pamoja na Rais wa timu Hersi Said na Ofisa Habari wa timu hiyo, Ally Kamwe pamoja na wachezaji wenzake.
Mechi ambazo Aucho akatazikosa ukiachana na ile ya jana dhidi ya Namungo ambayo Yanga ilishinda 3-1 ni pamoja na ya keshokutwa Jumatatu itakapoikabili Ihefu, Geita Gold na
Azam FC unaotarajiwa kupigwa Machi 17 jijini Dar es Salaam huku matokeo ya awali baina ya timu hizO ni Wanalambalamba kubamnizwa nmabao 3-2.