Prince Dube Ataja Ushirikina Chanzo cha Majeraha Yangu Azam FC

 

Prince Dube Ataja Ushirikina Chanzo cha Majeraha Yangu Azam FC

 Prince Dube Ataja Ushirikina Chanzo cha Majeraha Yangu Azam FC

Prince Dube anapata shaka juu ya majeraha yake tangu afike Azam FC anadhani kuna kitu kimejificha nyuma yake pale anaposema;


“Kitu kingine unayoweza kuiona any ninayoiona ni suala la majeraha yangu, ukiangalia majeraha yangu nikiwa Afrika Kusini au Zimbabwe utaona nilikuwa nacheza mechi zote za msimu mzima.


"Nilipokuja hapa sina muendelezo, nacheza mechi chache nakuwa nje nacheza tena mambo yanapoanza kuwa vizuri narudi tena nje, wakati napojaribu kukaa chini na kufikiria naona kuna kitu nyuma ambacho siwezi kukiona kwa hiyo nafikiri nikipata changamoto nyingine, mazingira tofauti huwezi kujua labda mambo yatabadilika, kwa kuwa mimi ni mchezaji ambaye anataka kucheza kila mechi, kuwa tayari kwa ajili ya timu, sasa vitu kama hivyo vikiendelea kutokea unaona hapana hapana hapa sio mahali pa kuendelea kuwepo, hivyo,” anasema Dube, mchezaji wa Azam FC matajiri wa Chamazi ambaye anapigania kutaka kuondoka kwenye klabu hiyo.


Dube baada ya kusema viongozi wa Azam FC wanazipenda Simba na Yanga kiasi inafika wakati wanashangilia timu hizo zikishinda au Azam FC inapopoteza, akasema pia timu hiyo haina malengo ya kushinda vikombe na kwamba tunavyoiona nje sivyo ilivyo ndani, yeye anataka kushinda vikombe kwahiyo anataka kuondoka akashinde vikombe kwingineko.


Leo anasema amekuwa majeruhi kwa muda mrefu na kila akirudi anapata majeraha mapya, anadhani kuna “ULOZI” unafanyika kwake ili apate majeraha, haikuwa hivyo alipokuwa Afrika Kusini au kwao Zimbabwe, ambako alikuwa anacheza karibia mechi zote za msimu, anataka kuondoka ili kuachana na hayo mazingira anayoyaona kama kuna ULOZI.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.